Muigizaji Elizabeth Michael (Lulu), amesema kesi inayomkabili ya kuua bila ambayo inamkabili haikuwahi kuisha kama baadhi ya watu wanavyodhani.
Muigizaji huyo huyo anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo bila kukusudia cha aliyewahi kuwa muigizaji mwenzie, Steven Kanumba kilichotokea April 7, 2012 . Akizungumza na Planet Bongo ya EA Radio ameeleza kuwa watu wanadhani kesi hiyo ilimalizika kutokana na kutojua sheria.
“Unajua watu hawajui sheria, kesi haikuwahi kuisha ni procedure ya kawaida ya mahakama imefuatwa na ni muda wake umefika sasa, siyo kama imeibuka tu” amesema Lulu.
“Kwa sababu mimi ndiye muhusika nimepata taarifa kwa njia ya kisheria siyo kama nyie kwenye mitandao, pengine niliipata kabla yenu” ameongeza.
Hata hivyo amesema kuwa asingependa kulizungumzia sana suala hilo kutokana tayari lipo mahakamani ila amelazimika kufanya hivyo kutokana yeye ndiye muhusika. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena hapo kesho October 19, 2017.
No comments:
Post a Comment