Rais wa Guatemala Jimmy Morales ameamrisha ubalozi wa nchi hiyo nchini Israel kuhamishwa kwenda Jurusalen.
Katika ujumbe kupitia Facebook, Bw. Morales alisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kuzungumza na waziri mkuu Benjamin Netanyahu.
Wiki iliyopita Guatemala ilikuwa moja ya nchi tisa zilizopiga kura kupinga azimio la Umoja wa Mataifa la kuitaka Marekani kufuta hatua ya kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Donald Trump alitishia kupunguza misaada kwa nchi ambazo zilipiga kura dhidi ya Marekani, Marekani ni mtoaji muhimu wa misaada kwa Guatemala, nchi maskini ya kati kati mwa Amerika.
Siku ya Jumapili Bw. Morales alisema kuwa alikuwa ameamrisha mmlaka za nchi hiyo kufanya mikakati ya kuhamisha ubalozi kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.
Hali ya mji wa Jerusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestiona, Israel ilitwaa mji huo ambao awali ulikuwa ukikaliwa na Jordan wakati wa vita vya mwaka 1967 vya Mashariki ya Kati na inaitaja mji wote huo kuwa mji wake mkuu.
Wapalestina wanadai kuwa East Jerusalem ni mji wao mkuu taifa lake la baadaye, Jerusalem haujatambuliwa kimataifa na nchi zote kwa sasa zina balozi zao huko Tel Aviv.
No comments:
Post a Comment