Translate

Friday, July 9, 2021

USICHOKIJUA KUHUSU ZAO LA KAHAWA

Kahawa (Coffee) ni kinywaji Cha tatu kinachonyweka zaidi Duniani baada ya maji na  chai. Na kama ulikuwa hujui pia ni Kuwa Kahawa ni bidhaa ya pili  inayouzwa zaidi Duniani (Most traded commodity) baada ya Mafuta (Crude Oil).



Nchi maarufu Kwa uuzaji kahawa Duniani ni Brazil ikifuatiwa na Vietnam.

Monday, July 5, 2021

MANARA AAHIDI KUACHA KAZI SIMBA IKIFUNGWA KIGOMA

Anaandika  *HajiSManara* Unafika Pemba kutokea Airport hadi kinyasini Wete Pemba kote barabarani watu wametinga jezi za Mnyama. 



Wapemba hawajali kuhusu matokeo ya juzi,,before sikuwa najua Pemba ina Simba wengi kiasi hiki aiseee. 

 

NDEGE ZA ZIMAMOTO ZAPELEKWA KUSAIDIA CYPRUS

Cyprus seeks Israel, EU help to fight wildfire

Umoja wa Ulaya umetuma usaidizi wa angani kusaidia katika kudhibiti moto mkubwa wa msituni unaosambaa katika miji ya kaskazini mwa Cyprus ya Limassol na Larcana.

Mkuu wa Umoja huo pamoja na Tume ya Umoja wa Ulaya, wamesema ndege za kuzima moto zimetoka Ugiriki kwenda kupambana na moto huo ambao maafisa wa Cyprus wanasema ni mbaya zaidi katika rekodi yake.

PAPA FRANCIS ALAZWA..

 Papa Francisko Alazwa Hospitalini Kwa Operesheni Kubwa, Roma!

Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 4 Julai 2021 majira ya jioni amelazwa kwenye Hospitali ya Gemelli iliyoko mjini Roma kwa ajili ya kufanyia operesheni kubwa kwenye utumbo mpana. Operesheni hii inafanywa na Prof. Sergio Alfieri. Baada ya operesheni, Hospitali ya Gemelli itatoa taarifa kuhusu hali ya Baba Mtakatifu Francisko. Jumapili mchana amesali na waamini Angelus

Saturday, July 3, 2021

NI VIZURI WOTE TUPATE CHANJO -MULAMULA


Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Liberata Mulamula amesema


 amefurahishwa na ushauri wa wataalamu wa afya katika mikakati ya kisayansi ya kupambana na ugonjwa wa Corona. 


Wataalamu hao wa ndani walipendekeza matumizi ya njia za kisayansi kujikinga na Corona ikiwemo chanjo na kuvaa barakoa.


Waziri Mulamula amesema ni vyema watanzania wote wakapatiwa chanjo ili kuwa salama na kuondokana na sharti la kuvaa barakoa kama ilivyo kwa raia wa Marekani ambao wameshachanjwa.


Ameyasema hayo Dodoma alipozungumza na @dar24news