Translate

Thursday, September 17, 2015

NCCR -MAGEUZI MGUU NJE MGUU NDANI UKAWA


Sintofahamu imeibuka ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi ambapo viongozi wake wamedai kuwa taratibu zilizo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) zimekiukwa na kufanya chama hicho kuingia katika mgogoro wa majimbo

 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho,Leticia Ghati Mosore amesema  kuwa NCCR-Mageuzi wamezidiwa idadi ya majimbo kutokana na taratibu nyingi kukiukwa kuanzia serikali ya Mtaa na sasa uchaguzi Mkuu.

 Mama Mosore amesema baada ya kuona mambo hayaendi sawa, na ingawa wataendelea kuwa UKAWA, lakini sasa wameamua kupambana wenyewe kama NCCR-Mageuzi katika kugombea viti vya ubunge pamoja na udiwani katika mgawanyo huo ambao amedai chama hicho kimepata majimbo pungufu ndani ya umoja wa vyama vinavyounda Ukawa

Amesema kuwa ili kukamilisha ushirikishwaji kulitakiwa kuundwa kamati zitakazoendesha uchaguzi ndani ya UKAWA na mambo mengine mengi ikiwemo uwazi wa matumizi ya fedha, lakini hayajaweza kufanyika hivyo

Mchakato wa kumpata mgombea Urais haukufuta utaratibu katika ushirikishwaji wa vyama vyote vitakavyoweza kutambua mgombea gani anaweza kusimama katika kupeprusha bendera ya UKAWA”, amesema Mama Mosore.

Mama Masore pia ametaka Mwenyekiti wao Mhe. James Mbatia asiwe msemaji wa CHADEMA wakati anakiacha chama chake (NCCR-Mageuzi) kinadhoofika, akidai kwamba wananchi wanashindwa kututoufautisha UKAWA na CCM na wataamua kuchagua zimwi walijualo. “Tunasisitiza upinzani wa kweli nchini hauwezi kujengwa kwa njia za hila, kwa kukiuka taratibu za kidemokrasia, tutachangishana ili tusafiri kwenye majimbo na kata za wagombea wetu na kuwasaidiaalisema

Mama Masore amesemaTunamshauri Mwenyekiti James Mbatia aitishe vikao vya kikatiba haraka  ili tuweze kujadiliana kuhusu hatima ya Chama chetu.Upinzani wa kweli haujengwi kwa kuweka mbele tamaa na maslahi binafsi kuliko taifa, na kwa kutegemea propaganda. 

 “Tangu UKAWA ianze, matokeo yake yamekuwa ni mabaya kwa uhai na ustawi wa Chama chetu cha NCCR”, amesema mama Masore

 Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Chama hicho,Bw. Mosena Nyambabe amesema kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuwa ndio kinafanya uandaji wa masuala yote bila kuwa na ushirikiano na NCCR-Mageuzi licha kuwa na udogo katika muungano huo

 Bw. Nyambabe amewataka wanachama wote wa NCCR-Mageuzi kushikamana katika uchaguzi mkuu ili kupata majimbo hayo licha ya kuwepo kwa changamoto ya kufanyiwa vurugu na Chadema. Bw. Nyambabe amehoji juu ya hatima ya NCCR-MAGEUZI baada ya uchaguzi na UKAWA wakiwa madarakani huku changamoto zikiwa bado hazijamalizika, akitolea mfano itakuwaje kwenye mgawanyo wa wakuu wa mikoa ,pamoja na wakuu wa Wilaya

 Amesema NCCR-Mageuzi imepoteza matumaini katika muungano huo ya kupata wabunge wengi, na kusisitiza kuwa chama hicho kitakuwa na wakati mgumu bila kutafuta ufumbuzi kukiwa bado mapema 

Mgawanyo wa majimbo ambao unaleta mkanganyiko katika UKAWA ni ChademaMajimbo 148; CUF (Majimbo 99) ,NCCR-Mageuzi (Majimbo 12) na NLD - Majimbo matatu.

No comments:

Post a Comment