Hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya Bunge; Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda amefariki leo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Balozi Kijazi amethibitisha taarifa hizi na familia imethibitisha kutokea kwa msiba huu.
Apumzike kwa amani
=======
UPDATES:
Toka Serikalini:
Kwa maskitiko makubwa serikali inatangaza Kifo Cha Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda MB. Waziri wa Viwanda na-Biashara kilichotokea katika Hospitali ya Apollo, New Delhi India leo.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu pamoja na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu-na mazishi- zitaendelea kutolea na serikali hapo mbeleni.
Sisi wote ni wa mwenyezi na kwake- tutarejea.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo.
No comments:
Post a Comment