Translate

Wednesday, October 28, 2015

UKAWA HAWATAMBUI MATOKEO YA URAISI YANAYOTANGAZWA NA TUME

Mwenyekiti mwenza wa UKAWA mh Freeman Mbowe amesema hawatambui matokeo ya urais yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kwa madai ya kuhujumiwa.

Mbowe alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa ngome Kawe.

Aidha amelalamikia kukamatwa kwa vijana wa IT pamoja na raia wa kigeni ambao amesema hawahusiani na CHADEMA.

Mbowe ametumia muda mrefu kulalamikia kuvurugwa mfumo wao wa vijana wa IT.
Amesema hata CCM wamekuwa na vijana kama wa namna hiyo ambao wanakusanya matokeo na kuchakachua.
Kesho amesema watakutana kamati kuu ya CHADEMA, na pia viongozi wanaouda UKAWA.

No comments:

Post a Comment