Staa wa muziki kutoka Nigeria amepata mtoto wa pili kwa mujibu wa blogs za udaku nchini Nigeria. Wizkid ambaye alikuwa na mahusiano na mwanamke kutoka Guinea ‘Binta Diamond Diallo’ amejifungua mtoto wao wiki hii.
Wizkid na Binta walishawahi kupigwa picha wakiwa pamoja wakati WizKid yupo Marekani. Mtoto huyu ambaye ametajwa kuwa ni wa WizKid amepewa jina Ayodeji Ibrahim Balogun kama jina halisi la baba yake Ayodeji Ibrahim Balogun aka WizKid.
Mpaka sasa WizKid hajasema lolote kuhusu issue hii.
No comments:
Post a Comment