Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje, Peter Msigwa amesema Rais John Magufuli ameshindwa kutumia nafasi muhimu ya kuitangazia dunia msimamo na mwelekeo wa Serikali yake kwa kutohudhuria sherehe ya mwaka mpya wa mabalozi iliyofanyika Ikulu mapema wiki hii.
Licha ya sherehe hiyo fupi ya mabalozi waliopo nchini kufanyikia Ikulu, Rais alimtuma Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga kumwakilisha, jambo ambalo limekosolewa na wengi.
Mchungaji Msigwa, ambaye ni mbunge wa Iringa Mjini, alisema hayo juzi usiku wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Channel Ten.
“Ulikuwa ni wakati mwafaka kwa Rais kubainisha msimamo wake juu ya masuala kadhaa na nchi tunazohusiana nazo. Ilikuwa ni fursa kwa yeye kutoa uelekeo wa Serikali yake na aina ya uhusiano autakao,” alisema Mchungaji Msigwa.
Msigwa alimsifu Dk Magufuli kwa mwanzo mzuri wa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuoongeza uwajibikaji serikalini, lakini akasema maendeleo endelevu hupatikana kwa ushirikiano na wadau mbalimbali, zikiwamo nchi jirani na marafiki.
Alisema utafika wakati Rais atalazimika kwenda kusalimia na kujitambulisha kwa marais wa nchi jirani ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nyinginezo; ndani na nje ya Afrika.
“Hawa wote walishirikiana vyema na mtangulizi wake na walikuwa na mipango mingi ambayo ama inaendelea au haijatekelezwa bado. Lazima aende huko ili kutekeleza masuala yote muhimu kwa Taifa,” alisisitiza.
Alikumbusha kuwa mikutano kama hiyo ni ya kitamaduni kwani imekuwapo tangu enzi za Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliitumia kutoa msimamo wa Tanzania dhidi ya masuala kama ubaguzi wa rangi, uhuru wa mataifa ya Afrika vita dhidi ya umasikini na tofauti ya kipato.
Mikutano ya kimataifa
Miongoni mwa mambo ambayo yatamlazimisha Rais Magufuli kutoka nje ya mipaka ya Tanzania, kwa mujibu wa Mchungaji Msigwa, ni pamoja na kuhudhuria mikutano mikubwa ambayo haihitaji uwakilishi wa mtu mwingine yeyote zaidi ya mkuu wa nchi husika. “Ipo mikutano ambayo hata akina (Rais wa Urusi, Vladimir) Putin au (Rais wa Marekani, Barack) Obama hawakosi. Ni marais pekee wanatakiwa kuhudhuria ili kutoa misimamo ya nchi zao. Huko ni lazima ataenda.”
Alisema hayo huku akinukuu kauli iliyowahi kutolewa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mpaka kuwa Tanzania inayohitaji mataifa mengine kuliko yenyewe yanavyoihitaji Tanzania na kueleza kuwa hilo lina maana kubwa kwenye uchumi wa nchi.

No comments:
Post a Comment