Translate
Tuesday, March 29, 2016
LOWASSA: WATANZANIA DUMISHENI AMANI
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani nchini ili kutekeleza maagizo wanayopewa na viongozi wa dini.
Lowassa aliyasema hayo jana katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front jijini Dar es Salaam, wakati wa ibada maalumu ya shukrani. Katika ibada hiyo, Lowassa aliambatana na familia yake na viongozi mbalimbali wa dini na vyama vya siasa.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria ibada hiyo, ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji; Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR –Mageuzi, James Mbatia.
Wengine ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Paul Ole Mameo; Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment