Translate

Monday, May 30, 2016

SERIKALI KUPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI PAMOJA NA POMBE YA ILIYOFUNGWA KWENYE MIFUKO MAARUFU KAMA VIROBA

May 26 2016 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba imepiga marufuku moja kwa moja, utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini kuanzia mwaka 2017 hii pia inahusu matumizi ya mifuko ya plastiki inayofungia pombe maarufu kwa jina la viroba.


Waziri Makamba ameeleza kuwa mifuko ya plastiki imekuwa na changamoto kubwa ya mazingira kwa kuwa sehemu kubwa ya mifuko hiyo hutolewa bure na inasambaa na kuziba mifereji hivyo husababisha mafuriko na athari nyingine kubwa kwa mzazingira.

Waziri Makamba ameongeza kuwa ofisi yake inakamilisha majadiliano ndani ya Serikali na baadae kuwahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku moja kwa moja matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Serikali itatoa muda kwa waliojiajiri na kuajiriwa na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hizo na itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungio mbadala’

Tumetuma wataalamu wa Serikali katika nchi zilizofanikiwa kwenye jambo hili ili kujifunza namna bora ya kulitekeleza‘

Waziri Makamba ametoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko ya plastiki waanze kujiandaa sasa kwa zuio hilo.

No comments:

Post a Comment