Akielezea Miradi hiyo yote Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mhandisi Modest Aporinali amesema bajeti ambayo waliyonayo kwa kila kituo cha afya wametenga kiasi cha sh ,Milioni Mia moja na kwamba mahitaji ni vituo vya afya kumi na kwasasa ni vituo viwili ambavyo vinafanya kazi.
“Ni kweli Halamshauri yetu ina uhitaji mkubwa sana wa Vituo vya afya ingawa kwa sasa tunavyo vituo viwili ambavyo ni Nyankumbu na Kasamwa ambavyo vinafanya kazi, hata hivyo mmeona tumezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye vituo vitatu ambapo ni Mpomvu,Nyanguku na Shiloleli tutaendelea na jitihada kwa kutumia mapato yetu ya ndani ili kupunguza changamoto ya vituo vya afya hata hivyo GGM wametupa msaada kama milioni mia moja kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mgusu”Alisema Modest. Picha kwa hisani ya Madukaonline
No comments:
Post a Comment