Translate

Saturday, May 20, 2017

VIONGOZI 190 WA JUBILEE WATANGAZA HALI YA HATARI KWA KENYATTA



Maafisa wa chama cha Jubilee kutoka mojawapo wa ngome za Uhuru Kenyatta wametishia kuhama chama - Maafisa hao wanakishutumu chama kwa kukaliwa na baadhi ya watu - Sasa wanampa ilani kiongozi wa chama Uhuru Kenyatta, la sivyo watatafuta njia zingine Chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta kinakabiliwa na wakati mgumu
, hii ni baada ya maafisa wake 190 kutoka eneo la Mlima Kenya, kutishia kukihama.  Viongozi hao, wamemnyooshea kidole cha lawama Katibu Mkuu wa chama hicho Raphael Tuju, ambaye wanadai anakiendesha chama hicho kwa manufaa ya watu wengine huku viongozi wa Kaunti wakidharauliwa na ambao ni nguzo muhimu katika kushughulikia maeneo yaliyotengwa katika Kaunti ndani ya chama. Kwenye kikao na wanahabari Alhamisi, Mei 18, Mwenyekiti Alhaji Mwendia aliionya serikali ya Jubilee dhidi ya kuingilia kampeni katika eneo hilo.

“Watu kadhaa wamekuwa wakija katika Kaunti wakidai kufanya kampeni za Urais lakini hatuwajui ni kina nani. Juhudi zote za kupiga kampeni ya Rais ni lazima kushughulikiwa na maafisa wa kamati za tawi,” Alisema.
Pia alimtaka Rais kufanya hima na kukutana nao ili kutatua mgogoro uliopo licha ya kutoa ilani ya siku 7 kwa Uhuru kuwasilisha jibu. Aidha viongozi hao wametishia kuvamia Makao Makuu ya Jubilee jijini Nairobi ikiwa matakwa yao hayatashughulikiwa ndani ya siku7.

No comments:

Post a Comment