KUFUATIA sakata la mzazi mwenziye kuchepuka na kuzaa na mwanamitindo maarufu Bongo, mwanamke shupavu na mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’, amesema hakuna cha kumliza juu ya sakata hilo kwani akaunti yake benki imejaa mkwanja wa kutosha.
Zari alitoa povu kwenye komenti aliyomjibu shabiki wake ambaye alikuwa akimuonea huruma na kusema kwamba anajua kuwa ameumizwa sana na kitendo hicho cha ‘Baby’ wake kuzaa na Hamisa Mobetto, sema tu analilia kwa ndani.
Mpaka saa Zari bado hajaweka wazi kuwa ataendelea na mzazi mwenziye huyo ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, au atachukua hatua gani, ikiwa ni siku moja tu imepita tangu mzazi mwenziye huyo akiri hadharani kuwa mtoto wa Mobetto ni wake.
No comments:
Post a Comment