Mbali na Profesa Kitila ambaye alikuwa kada wa ACT, pia kuna Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Kitambi ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha, Lawrence Masha, Samson Mwigamba na Albert Msando.
Akizungumza mbele ya mkutano huo, Profesa Kitila amesema: "Nguvu ya CCM zipo tano, moja ni kwamba ni chama cha watu, ni chama pekee chenye nguvu siyo chama kuogopa watu, tulijaribu huko tulipokuwa lakini yalishindwa."
Kwa upande wake, Masha amesema alipoamua kuondoka, baba yake alisikitishwa na uamuzi huo lakini baada ya kutafakari ameamua kurejea nyumbani.
Amesema yeye ni mwanaCCM na kijana alilelewa ndani ya chama hicho.
"Mwenyekiti wewe ni mfugaji, ng'ombe akiingia zizini amekatwa mkia unamwangalia mara mbili mbili, mimi sijakatwa mkia ni mwaminifu, ukinihitaji nitumie, kudumu Chama cha Mapinduzi," amesema Masha.
Kwa upande wake Mwigamba amesema hoja zote walizopigania Rais John Magufuli kwa sasa anazitekeleza. Kutokana na hali hiyo analazimika kumuunga mkono.
"Lakini ni bahati mbaya wapo wanaoamini upinzani ni kama, tumeamua kuwa moto, wanaposema huyo amenunuliwa, mie ndiyo naendelea kuwa moto.”
Yeye Msando amesema baada ya kutoka Chadema kwenda ACT amejitambulisha rasmi kujiunga na chama hicho.
Amesema anafarijika kuona chama hicho na haoni aibu kuwa karibu na CCM tofauti na ilivyokuwa miaka ya zamani kwani wanachama walihofia kuvaa mavazi ya chama hadharani kwa kuogopa kuzomewa.
"Kwa sasa chini ya uongozi wako, mtu anajivunia kuwa mwanachama wa CCM, tukaona juhudi zinazoendelea," amesema Msando.
No comments:
Post a Comment