Mugabe alikubali ushauri huo lakini alikataa kukabidhi hotuba yake ya kujiuzulu kwa viongozi wa jeshi la nchi hiyo ili waihariri. Hata hivyo aliwahakilishia kuwa atajiuzulu. Lakini ametumia muda aliopewa kuhutubia taifa kusisitiza umoja na mshikamano wa taifa na kueleza umuhimu wa kusameheana na kusonga mbele.
Katika hali isiyotarajiwa amekataa kutambua maamuzi ya kumvua uenyekiti wa chama na amesisitiza kuwa ataongoza mkutano mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao "The congress is due in a few weeks from now. I will preside over its processes. People cannot ride roughshod over party rules and procedures." Amenukuliwa na shirika la habari la AP.
Mugabe amehitimisha hotuba yake bila kusema kama amejiuzulu au lah. Viongozi wa jeshi wamelaumiwa kwa kumruhusu Mugabe kuandaa hotuba hiyo ya kujiuzulu na kuisoma bila kwanza kupitiwa.
Kabla hajasoma hotuba hiyo uliibuka mgogoro kwenye ikulu ya nchi hiyo baada ya jeshi kumtaka akabidhi hotuba hiyo waipitie kwanza. Mugabe alikataa akiahidi kuwa atatangaza kujiuzulu wakati akihutubia. Lakini hadi anamaliza kuisoma hakuna popote alipotamka kujiuzulu wala kusema lini anatarajia kujiuzulu. Bado haijafahamika jeshi na chama cha ZANU-PF vitachukua hatua gani baada ya Mugabe kuwapiga chenga hiyo ya mwili.!
No comments:
Post a Comment