Translate

Friday, November 10, 2017

DIASPORA WAKUNWA NA KAZI YA MAKONDA.


Paul Makonda..

Jumuiya ya watanzania wanaoishi Diaspora (Marekani) ijulikanayo kama *Sixth Region Diaspora Caucus Washington* kwa pamoja wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam _*Mh Paul Makonda*_
kutatua changamoto za ofisi za walimu wa mkoa huu kwa kutoa *makontena 36* ya samani mbalimbali zikiwemo *viti vya kisasa zaidi ya 5000,meza za umeme 2500,meza za kawaida 2500,makabati ya vitabu makubwa 1300 na bao (writing boards) za kuandikia 700*. Mchango huu wa samani ambao una thamani ya zaidi ya dola za kimarekani *$ 800,000* ambazo ni sawa na *shilingi 1,800,000,000* za kitanzania utatumika katika ofisi mpya 402 za walimu zilizoanza kujengwa kupitia kampeni iliyoanzishwa na *_Mh Paul Makonda_* mapema Agosti mwaka huu. Kupitia samani hizi adhma ya *_Mh Paul Makonda_* ya kutengeneza mazingira rafiki ya utoaji wa elimu kwa walimu wa Mkoa wa Dar es salaam itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na matarajio ya kupandisha kiwango cha elimu...

No comments:

Post a Comment