Akiongea na waandishi wa habari mchana wa leo Mh Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza umoja wa katiba ya wananchi {UKAWA} amesema wamepokea barua ya kuzuia kutumia uwanja wa jangwani huku sababu kubwa ikitajwa kuwa utakuwa na matumizi mengine
Mh Mbatia amesema wamejaribu kila njia lakini imeshindikana ikiwemo pia kumuomba mkurugenzi wa jiji awaambie nani aliyekodi huo uwanja ili wafanye nae mazungumzo lakini amegoma kuwaeleza!
Mh Mbatia amewataka wanachama wote na wapenzi wa UKAWA kuwa watulivu huku viongozi wote wkifanya jitihada za kufanikisha zoezi hilo
Awali ufunguzi wa kampeni za uraisi kupitia mgombea anayepigiwa chapuo na UKAWA ulikuwa umepangwa kufanyika jumamosi trh 29 august kwenye uwanja wa Jangwani!
No comments:
Post a Comment