Translate

Thursday, August 27, 2015

WAZEE WA CHOPA WAPIGWA MKWALA NA TCAA!

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema kutokana na uzoefu wa nyuma kwamba katika kipindi cha kampeni za siasa, vyama vya siasa hutumia kila aina ya usafiri kuwafikia wananchi ambao ni wapigakura wao. Usafiri huo ni magari, pikipiki, baiskeli pamoja na ndege na helikopta kwa vyama vyenye ukwasi hivi sasa wanatakiwa kufanya yafuatayo. Watoa huduma za usafiri wa helkopta au ndege na marubani wake watakaokodishwa kutoa huduma wakati wa kampeni, wametakiwa kuzingatia kanuni za usafiri wa anga na kuomba kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania

No comments:

Post a Comment