Translate

Monday, September 28, 2015

GOLIKIPA WA TAIFA STAA AFARIKI KWENYE MKANYAGANO MACCA

 Kipa wa zamani wa Reli ya Morogoro na Taifa Stars, Hemed Mussa, amefariki dunia nchini Saudi Arabia.

Mussa aliyechezea Reli mwishoni mwa miaka ya 1980 na 1990, amefariki baada ya kutokea tukio la mahujaji takribani milioni mbili kukanyagana kwenye Mji wa Mina karibu kabisa na Makka wakati wakiwa kwenye hijja.

Marehemu Mussa alikuwa mmoja wa mahujaji Watanzania waliokwenda kuhiji na awali ilielezwa wanne kati yao walifariki kupitia taarifa ya Mufti, Abu Bakari Zubery ambaye yuko Makka.

Mmoja wa ndugu wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Said Mussa, alisema wamepata taarifa hizo kutoka kwa mwandishi wa redio moja nchini ambaye yuko hijja pia.

“Kweli ametueleza ndugu yetu amefariki dunia, hivyo tunaendelea kufuatilia zaidi kwa kuwa awali kulikuwa hakuna uhakika huo. Hatukuwa na uhakika, lakini sasa tumethibitisha,” alisema.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema: “Nilimjua vizuri sana marehemu, alikuwa kipa mzuri sana. Alikuwa mwajiriwa wa reli lakini mwenye kipaji uwanjani, ni masikitiko.”

Mahujaji wa Tanzania waliofariki na majina yao kutajwa kwamba ni miongoni mwa 717 waliofariki dunia ni Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman, Hemed na Sefu Said Kitimla.

No comments:

Post a Comment