Majira ya saa nne asubuhi vijana kadhaa ambao walikuwa wamevalia sare za chama cha CHADEMA na mabango kadhaa walionekana wakikatiza makao makuu ya chama hicho kwa mithili ya maandamano huku wakiwa wanachukuliwa picha na mwandishi wa gazeti la UHURU pamoja na mpiga picha wa Television ya STAR TV ambapo baada ya kufika makao makuu ya chama hicho walinzi pamoja na maafisa wa cham hicho walijipanga na kuwazunguka vijana hao ambao baadhi walikuwa na boda boda hali iliyowafanya vijana hao kutawanyika kwa kukimbia na kuvua t shirt za chama hicho ambazo walikuwa wamevalia juu ya nguo nyingine.
Baadhi ya kadi ambazo inadaiwa kukutwa nazo mwandishi huyo
Katika purukushani hizo waandishi waliokuwa wanawasindikiza waandamanaji hao akiwemo mwandishi wa gazeti la uhuru CHRISTOPHER LISSA pamoja na mpiga picha wa STAR TV waliwekwa chini ya ulinzi wa makamanda wa chama hicho kuwa kuhusishwa na kupanga tukio hilo ili wapate habari kuwa kuna maandamano lengo likiwa ni kukichafua chama hicho.
Mara baada ya kuwekwa chini ya ulinzi akiwemo mmoja kati ya vijana ambao alionekana kuchoka (TEJA) naye alikamatwa ambapo katika maelezo yake alikiri kupokea shilingi elfu kumi pamoja na T-SHIRT ya CHADEMA kutoka kwa vijana hao kwa lengo la kuambatana nao katika maandamano hayo ambayo hayakuwa halali.
Kwa mujibu wake anasema kuwa leo aliamua kufikia kinondoni kituo cha Manyanya kutafuta hao waandamaji na ndipo alipokutana na wenzake wa STAR TV na kisha watu ambao walikuwa wamepanga kuandamana kwalifika wakiwa na gari na kushuka na kuanza kupeana T-SHIRT za CHADEMA huku wakiwa ni kama wageni wa eneo hilo wakiulizia makao makuu ya chama kwa watu wengine.
Akizungumza na wanahabari afisa wa chama hicho BONIFACE JACOB amesema kuwa chama kilipata taarifa siku tatu nyuma kuwa kuna vikao vinakaa chini ya viongozi wawili wa CCM avikao ambavyo vilifanyika kurasini na ndipo chama kilijipanga kwa tukio hilo la leo.
Kwa mujibu wa afisa huyo anasema kuwa mwandishi huyo wa UHURU anahisiwa kushiriki kupanga maandamano hayo kutokana na kukutwa na kadi zaidi ya 20 feki za chama hicho ambazo walijipanga kujifanya kama zimerudishwa na wanachama hao kadi ambazo mwandishi huyo amekana kuhusika nazo
No comments:
Post a Comment