Translate

Sunday, October 4, 2015

MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI KWA AJARI YA GARI

Mwanasiasa mkongwe nchini Mch Christopher Mtikila amefariki asubuhi ya leo kwa ajari ya gari iliyotokea mkoani pwani

       Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema amefariki saa 12 kasorobo asubuhi katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.

Amesema gari lililokuwa limempakia lilikuwa linatokea Morogoro na kwamba walikuwa watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya.

Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya Tumbi.

No comments:

Post a Comment