Translate

Thursday, January 28, 2016

SUPERSTAA RIHANA KUACHIA ALBAMU YAKE WIKI HII


rihanna-anti-event
Rihanna
HAYAWI hayawi sasa yamekuwa. Baada ya kusubiliwa kwa muda mrefu, ile albamu mpya ya mwimbaji maarufu Rihanna “ANTI” imeripotiwa kukamilika na itaachiwa rasmi wiki hii.
rihanna-anti-event

Chanzo cha taarifa hiyo kimeiabia Billboard kuwa ANTI yenye nyimbo nane, iko tayari na kwamba muda wowote itaachiwa kabla ya Ijumaa (keshokutwa), Januari 29.
Awali, ANTI ilipangwa kuachiwa Mei au June mwaka jana lakini ikachelewa. Mwanzoni mwa wiki hii, Rihanna alianika kuwa albamu yake hiyo sasa iko tayari na kwamba imekamilika, aliandika kwenye mtandao wa twitter maneno haya “listening to ANTI”.
Rihanna anatarjia kuanza kufanya “ANTI World Tour”  Februari 26 wakati huo wimbo wake mpya “Work,” aliomshilikisha Drake, atauachia leo

No comments:

Post a Comment