DAR ES SALAAM: Mwigizaji wa sinema za Kibongo anayefanya vyema pia kwenye Muziki wa Mduara, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amedaiwa kumpindua mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa mpenzi wake, Ali Kiba ‘King Kiba’, Ijumaa Wikienda limenasa vielelezo vya ubuyu kamili.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, Sabby amevamia penzi la Jokate na kuhakikisha anampa ‘vitu adimu’ Kiba kiasi ambacho mkali huyo wa Wimbo wa Lupela kuhamishia majeshi rasmi kwa mrembo huyo ambaye jina lake linazidi kushamiri siku hadi siku mjini.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mpenzi wake, Ali Kiba ‘King Kiba’,
“Huwezi amini mtoto wa kike kampa mambo adimu Kiba kachanganyikiwa. Amehamishia kabisa majeshi kwa Sabby. Hana habari tena na Jokate kwa sasa, akili yake yote ipo kwa Sabby,” kilisema chanzo hicho.
Wakati chanzo hicho kikivujisha ubuyu huo, chanzo kingine kilikwenda mbele zaidi kwa kuanika mawasiliano ya kimahaba kati ya Kiba na Sabby.
Kwenye meseji hizo zilizoonekana kupigwa picha kutoka katika meseji halisi katika simu (screen shot), inaonesha namba iliyoseviwa jina la Kiba ikichati na ya Sabby wakiitana baby baby kwa sana huku wakichombezana na maneno matamu kuashiria ni ‘mtu na mtuwe’.
Kuna seheme Sabby anaonekana kumchombeza Kiba kwa maneno matamu; “be free, jiamini ati. Mimi si kama hawa malaya wa mjini. Ni mpenzi wako, napenda mwanaume anayenijali…”
Baada ya kunasa meseji hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Kiba bila mafanikio lakini bahati nzuri Sabby alipatikana na kukiri kuwa na uhusiano na Kiba lakini akaomba habari isiandikwe kwani hataki vitu hivyo vijulikane sababu haikuwa kusudio lake.
“Niliibiwa simu sasa nafikiri aliyeniibia ndiyo kawapa hayo mawasiliano yangu na Kiba. Please naomba msiandike hiyo habari, mtaniharibia,” alisema Sabby.
No comments:
Post a Comment