Translate

Saturday, August 20, 2016

BI SHAKILA HATUNAE TENA!

Mwimbaji Shakila Said enzi za uhai wake.
BI Shakila Said enzi za uhai wake
Mwimbaji mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Shakila Said amefariki dunia usiku wa jana baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbagala, Charambe jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtoto wa mwisho wa marehemu aitwaye Shani ni kwamba marehemu amefariki baada ya kudondoka ghafla alipotoka kuswali. “Mama hakuwa mgonjwa hata kidogo, aliswali swala ya magharibi vizuri na baadaye akadondoka na kufariki,” alisema Shani huku akilia.
Marehemu Shakila ameacha familia ya watoto 13

No comments:

Post a Comment