Translate

Sunday, August 21, 2016

SUDAN KUSINI YASAJILI WATOTO JESHINI

Tangu mwanzo wa mwaka huu watoto zaidi ya 650 wamesajiliwa na makundi yenye silaha nchini Sudan Kusini, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.

Shirika hilo linasema kuna hofu kwamba mapigano mapya yanaweza kuwawaweka maelfu ya watoto katika hatari kubwa.

Christophe Boulierac ambaye ni msemaji wa UNICEF ametoa wito wa kukomeshwa mara moja vitendo vya kuwaingiza watoto jeshini na kuwaachilia bila masharti watoto wote walio katika makundi yote yenye silaha.

Inakadiriwa kuwa watoto 16,000 wamesajiliwa na makundi yenye silaha na majeshi na kulazimishwa kushiriki vita tangu kuzuka kwa machafuko Sudan Kusini Desemba 2013

No comments:

Post a Comment