Kamanda Simon Sirro
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amewataka uongozi wa Clouds Media Group kushirikiana na jeshi la polisi katika upelelezi wa tukio la uvamizi wa kituo chao cha matangazo.
Akiongea na waandishi wa habari leo Sirro amesema kesi yoyote inahitaji ushahidi na uvamizi wa Clouds bado upelelezi wake unaendelea ukikamilika utapelekwa kwa wakili wa Serikali ili aone kama anaipeleka kesi hiyo mahakamani au kutoipeleka.
"Ndugu zetu wa Clouds watoe ushirikiano kwa mpelelezi wa kesi yao, wao wanataarifa za kutusaidia kukamilika kwa upelelezi ila nasi tuweze kuipeleka katika hatua inayofuata. Na sio kwamba tukio limesahaurika bali upelezi wake unaendelea," amesema Sirro.
Chanzo: mwananchi
No comments:
Post a Comment