Translate

Wednesday, November 18, 2015

BUNGE LA RWANDA LAIDHINISHA KAGAME KUGOMBEA MUHULA WA TATU

Bunge la Senate la Rwanda limeidhinisha
marekebisho katika katiba yatakayomuwezesha
rais Paul Kagame kugombea urais kwa muhula
wa tatu.
Bunge la ngazi ya chini lilipitisha azimio hilo
mwezi uliopita lakini ni lazima lipigiwe kura ya
maoni kabla ya kuidhinishwa kikamilifu.
Wafadhili wa kimataifa wameelezea wasiwasi
kuhusu hatua ya Rais Kagame kugombea urais
kwa muhula wa tatu baada ya kumaliza muhula
wa sasa mwaka 2017.
Rais Kagame amesifiwa kwa kujenga upya nchi
hiyo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994
lakini wapinzani wanasema amekuwa
akiwakandamiza wakosoaji wake.

No comments:

Post a Comment